KUHUSU
CHIEF NSOKA
MAI NDOMBE, DRC
"Tumekuwa na desturi ya kulinda misitu kila mara. Tangu kampuni ya kutengeneza mbao iondoke na tuanze kushirikiana na Wildlife Works, tumeshuhudia hali ambapo misitu inakua upya."
GILDARDO CALDERÓN
PUTUMAYO, COLOMBIA
"Tunategemea Dunia Mama yetu ili kupata bidhaa tunazohitaji kwa ajili ya familia zetu. Hiyo ndiyo maana ni wajibu wetu kutunza afya ya mazingira."
LOMBE ILLUNGU
ECO-GUARD, MAI NDOMBE DRC
"Ulimwengu unategemea maisha ya misitu."
JR BWANGOY BANKANZA
MKURUGENZI WA TAIFA WW, DRC
"Msitu ni mama yetu.
Tunapomlinda,
Naye pia anatulinda."
CHIEF BASABO
MAI NDOMBE, DRC
"Misitu ni chanzo cha maisha, tuliyorithi kutoka kwa mababu.
Jukumu langu ni kupitisha utamaduni wetu, ili tuweze kulinda misitu, ambayo ni utajiri wetu."
LAURA YAWANAWA
BRAZIL
"Njia yetu ya kuishi ni sehemu ya suluhu kwa janga la tabianchi."
Mike Korchinsky aliasisi Wildlife Works mwaka 1997 kwa wazo kwamba ikiwa tunataka wanyama pori katika ulimwengu wetu, juhudi za uhifadhi lazima zifaulu kwa wanajamii wanaotumia.
MAADILI YETU
TUNATHAMINI
HALI ANUWAI
Ya spishi
Ya mbari na utamaduni
Ya jinsi na mwelekeo ya kingono
Ya maon
USAWA NA UHURU
Ili kuisha maisha bila kugandamiza wengine
Kufanya maadili na desturi zako za kimaadili kuheshimiwa
Kubaini binafsi mustakabali wako
Ili kusema mawazo yako, ilimradi usemi huo si wa kuendeleza vurugu au kunyima wengine uhuru
Kila mtu ana simulizi lake, ambalo linastahiki kupewa fursa ya kusikilizwa na kutambuliwa.
TUNATHAMINI
TUNATHAMINI
TUNATHAMINI
TUNATHAMINI
TUNATHAMINI
TUNATHAMINI
UWAJIBIKAJI
Binafsi na wa pamoja
UADILIFU NA UWAZI
Uwazi ni muhimu katika kujenga uaminifu. Hakuna chochote kilicho muhimu kuliko uaminifu katika kuvumbua upya jamii zetu.
ARI NA KUJITOLEA
Inayotokana na upole, heshima na ukarimu.
KUFIKIRI KIBUNIFU
Janga la tabianchi linahitaji suluhu nyingi, na tunaamini iliyo kamilifu haipaswi kuwa adui wa iliyo sawa.
UWEZO WA KUBADILISHWA
Na kufikiri kwa jumla katika ulimwengu huu changamano unaobadilika kila kuchao.
TUNAAMINI
Tunaamini kwamba viumbe vyote vina haki ya kimsingi ya kuishi Duniani.
Tunaamini kuwa watu wote wana haki ya kuhisi kuwa salama katika makazi yao ya jadi, kulea na kuelimisha watoto wao na kuazimia kupata maisha bora au kuenzi maisha ambayo wanayo tayari.
Tunaamini kuwa kwa kuendelea, kanuni hizi mbili zitagongana huku jamii za binadamu zikipanuka kwenye misitu zikitafuta makao mapya au mapato, na kuanza kushindana na wanyama pori kutafuta maji, chakula na matumizi ya maliasili.
Tunaamini kuwa tuna haki ya kunenea wale walio katika hatari kubwa ya mzozo baini ya binadamu na wanyama pori katika ulimwengu unaoendelea.
Tunaamini katika kutafuta suluhu zisizo za vurugu, na kwamba bunduki huchochea vurugu zaidi, kwa hivyo Walinzi wetu wa Wanyama pori hawabebi silaha (lakini wako imara na hawaogopi).
Tunaamini kuwa wengine wetu ambao viwango vyetu vya maisha vimepigwa jeki kupitia matumizi ya maliasili kutoka ndani ya misitu, tumekuwa wadau wakuu katika kuendeleza mzozo.
Tunaamini kuwa sasa tunafahamu athari ya vitendo vyetu, na kwamba sasa tuna chaguo la kuwa sehemu ya suluhu, ili kuwapa wale wanaoishi misituni njia endelevu, inayofaa wanyama pori ya kunawiri.
Tunaamini kuwa kiwango tu soko hudidimiza michango ya hisani, kwa hivyo hisani haiwezi kurekebisha kile ambacho kinaendelea kuharibiwa na soko.
Tunaamini kuwa soko si adui haswa, ni wewe na sisi, na tunaweza kuchagua biashara yenye uwajibikaji na kuelekeza nguvu za soko ili kusaidia kutatua matatizo badala ya kuyaanzisha.
Tunaamini kwamba suluhu zinazotegemea kazi na soko kama zetu zinapaswa kutolewa na biashara zenye uendelevu binafsi sokoni, ili tusidhibitiwe na mkataba finyu wa NGO, na tuweze kutekeleza mifumo ya jumla ya kukidhi mahitaji ya jamii za misitu huku tukilinda wanyama pori wakati huo kwa wakati mmoja.
Tunaamini katika uwazi haswa, ili uweze kutuwajibisha kwa vitendo vyetu, kusherehekea ufanisi wetu na kutambua changamoto zetu.
TUMEJITOLEA
KULINDA
VIUMBE ANUWAI
KUUNDA KWA PAMOJA NA WASHIRIKA WA JAMII
MAONI
YANAYOLINGANA NA MAZINGIRA
SULUHU
ZA SOKO
UWAZI
KULETA UFADHILI
WA MOJA KWA MOJA KWA JAMII
USAWA
KATIKA KUFIKIA
JAMII
HAKI NA MATAMANIO BINAFSI
USHIRIKIANO WA
SEKTA NA WASHIKADAU MBALIMBALI