KWA SERIKALI
Soko la Kujitolea la Hewakaa ni fursa
ya kimkakati kwa serikali mwenyeji:
kufikia fedha za tabianchi kwa masharti yao binafsi
kufanya kazi na sekta ya kibinafsi kama washirika sawa, si wafadhili
kutumia uhifadhi wa misitu kufadhili maendeleo ya matamanio binafsi huku zikichangia katika tabianchi ya dunia na malengo ya uendelevu
kufadhili maendeleo ya kitaifa na mitaani katika kiwango ambacho ni cha mageuzi na chenye athari za vizazi
Kwa nini ushirikiane nasi?
Wildlife Works inaongoza katika kuunda miradi iliyoanishwa ya REDD+ ambayo inahakikisha kuwa nchi wenyeji zinaweza kutumia mbibu za ufadhili kukidhi malengo yao ya sera, tabianchi, uhifadhi na maendeleo.
Tuna uzoefu wa miaka 25 hali ambayo imetufanya tuwe mshirika wa kuaminiwa na jumuiya za misitu na serikali.
Kama wataalamu wanaotambuliwa kote duniani katika REDD+, sisi ni washauri wanaoaminiwa na serikali ambazo vingependa kufuata mfumo wa kitaifa wa REDD+ unaoanisha miradi kwenye mpango wa kimaeneo.
Tuliwezesha utiaji sahihi wa ERPA kati ya Hazina ya Hewakaa ya Benki ya Dunia FCPF na Serikali ya DRC, na kufanya Mpango wa Ndombe ER kuwa mpango wa kwanza duniani kufaulu katika kuoanisha mradi ndani ya mpango wa kimaeneo.
KAMPUNI INAYOENDESHWA NA MAADILI
Mfumo wetu wa ugavi wa mapato unalenga kuwezesha malengo ya nchi wenyeji ili kutoa maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa jamii za ndani kupitia makubaliano ya ugavi wa mapato kwa usawa, huku tukifadhili matamanio ya nchi wenyeji kuingia katika mpwito wa kawi safi.
MCHAKATO NYUMBUFU ULIOFAFANULIWA VYEMA
Tuna mchakato ambao umejaribiwa na wa kweli wa maendeleo na utekekelezaji wa mradi unaotuwezesha kufanya mambo kulingana na mahitaji na utamaduni wa kila eneo huku pia ukifanya kazi kwa ufanisi kuanza kuzalisha mapato kutokana na mradi kwa ajili ya washirika wetu wa ndani ya nchi.
MAUZO NA UFADHILI THABITI
Tuna mkakati wa kipekee na wa moja kwa moja wa mauzo kupitia kampuni yetu ya kipekee ya mauzo, Everland Marketing ambao hutambua na kujenga mahusiano ya muda mrefu na wateja na wawekezaji wa kishirika walio na ari kuhusiana na tabianchi.
MISINGI MIPANA NA YA UFANISI
Tuliunda njia mpya kabisa ya ugavi wa msingi ambayo inasambaza Viwango vya kitaifa vya Uchafuzi wa vya Marejeleo ya Misitu (FREL) kulingana na hatari ya ukataji wa miti siku zijazo. Njia ya kuoanisha miradi kwenye mipango ya kimaeneo hukakikisha kuwa serikali za kitaifa zinaweza kutumia kwa ufanisi Soko la Kujitolea la Hewakaa ili kuweka pamoja ufadhili wa kifedha katika maeneo ya misitu yenye hatari kubwa zaidi huku zikichangia Michango Iliyobainishwa Kitaifa.
Soma zaidi kuhusu mbinu yake katika Mfumo wetu wa Desturi Njema nchini DRC.