KUHUSU MWAASISI WETU
UNGEPENDA KUPATA TAALUMA KUPITIA KWETU?
Tazama Jukwaa letu la Kazi
SIMULIZI LA CHIMBUKO LA WILDLIFE WORKS
TAZAMA
"Suluhu za jadi za tabianchi kote duniani zina msingi kwenye ukosefu wa usawa kwa jamii za ndani zilizo Kusini mwa Dunia. Tayari zimepata matatizo sana kutokana na mabadiliko ya tabianchi na tumejitolea kuhakikisha kuwa zipo kwenye mstari wa mbele wa kutafuta suluhu za tabianchi."
Mike Korchinsky
MWASISI NA RAIS WA WILDLIFE WORKS
Mnamo 1986, Mike pamoja na wengine waliasisi na kujenga mojawapo ya kampuni kubwa za ushauri kuhusu usimamizi nchini Marekani. (Axiom Management Consulting) ambayo iliuzwa mnamo 1995 kwa Cambridge Technology Partners (Novell), kampuni ya NASDAQ. Axiom iliangazia zaidi Uwekaji Upya wa Biashara, mchakato wa kibiashara wa kusaidia mashirika 1,000 kuunda upya utendakazi wa biashara zao ili kuzifanya ziwe za haraka zaidi, nyumbufu zaidi na ziweze kuwezesha ukuaji wa faida.
Katika ziara yake nchini Kenya mwaka 1996, Mike aligundua kuhusu mgogoro kati ya wanyama pori na jumuiya za mashinani. Hali hiyo ilimfanya kufikiria kuhusu njia za ufanisi za kutatua tatizo hili, na hatimaye aliweka mpango ambao ungelinda wanyama pori kwa njia ya kipekee na ya moja kwa moja; kwa kuwapa watu walio katika maeneo yenye wanyama pori wengi na shughuli mbadala endelevu za kiuchumi badala ya ujangili na kufyeka na kuchoma kilimo.
Mike aliasisi Wildlife Works mwaka 1997 kwenye msingi kwamba mahitaji ya wanyama pori lazima yasawazishwe na hitaji la kazi kwa jamii za ndani ambao wanyama ni sehemu ya mazingira yao.
Aliafuta eneo lenye kiwango cha juu cha mgogoro kati ya jamii na wanyama pori ili kufanyia mfumo wake mpya jaribio bora. Mike alianzisha eneo la uhifadhi la Wildlife Works lililoitwa Rukinga Santuary Kusini Mashariki mwa Kenya katika mkondo wa njia ya wanyama pori kati ya Mbuga za Kitaifa za Tsavo Mashariki na Tsavo Magharibi, maarufu kama Kasigau Corridor. Kwenye ukingo wa Rukinga Sanctuary, Mike alijenga kiwango cha kimazingira ili kuzalisha mavazi endelevu. Nafasi za ajira zilibuniwa kutokana na juhudi za uhifadhi na kiwanda cha mazingira, na punde si punde, idadi ya wanyama pori ilianza kuongezeka na kunawiri.
Mwaka 2008, katika kuitikia masuala yaliyoibuka kutokana na mpango wa REDD+ wa Umoja wa Mataifa (ambapo masoko ya hewakaa yangekuwa na nafasi katika kufadhili shughuli za kuhifadhi misitu) Mike alizindua asasi mpya, Wildlife Carbon LLC, ili kutafuta njia za upanuzi zaidi na wa haraka wa mfumo wa Uhifadhi wa Wildlife Works kupitia mauzo za hewakaa ya REDD+. Kutokana na hayo, mradi wa REDD+ wa Kasigau Corridor ulikuwa wa kwanza wa REDD+ duniani kutoa malipo ya mauzo ya hewakaa ya REDD+ chini ya Viwango vya Kuthibitisha Hewakaa (VCS) vinavyotambuliwa kimataifa. Tunaendelea kukuza shughuli zetu za miradi ya ubora wa juu wa REDD+ barani Afrika, Asia na Marekani ya Kati na Kusini, ili kulinda hekari milioni 5 ya misitu asili ambayo itapunguza tani milioni 25 ya uchafuzi wa CO2 kila mwaka na kuunda maelfu ya ajira endelevu.
Mwaka 2012, Mike alianzisha Code REDD, shirika lisilo la faida ambalo lengo lake ni kusaidia na kuboresha mbinu ya REDD+ ili kufikia uwezo wake kamili; kuwezesha watu, kuhifadhi misitu, kulinda wanyama pori na kupunguza uchafuzi. Chini ya uongozi wa Mike, Code REDD ilizindua mpango wake kwa watumiaji, Stand for Trees, ili kutoa uhamasisho kuhusu athari ya kulinda misitu na kutoa jukwaa la kuchukua hatua.
Akiwa na uzoefu wa zaidi ya miaka 20 ya kufanya kazi moja kwa moja na serikali za nchi zinazoendelea, sekta ya kibinafsi na jamii za ndani katika kutekeleza miradi ya kuhifadhi, Mike ameongoza Wildlife Works kuwa mojawapo ya mashirika yanayoongoza duniani kutekeleza REDD+.
Mike ni raia wa Kanada ambaye, wakati hasafiri ili kuzuru misitu iliyo hatarini ya dunia, ni mkaazi wa California Kaskazini. Ana shahada ya kwanza katika tasnia ya Uhandisi wa Kemikali kutoka Chuo Kikuu cha Birmingham, Uingereza.