top of page

-Joseph Mwakima

WILDLIFE WORKS AFISA WA MAHUSIANO YA JAMII

Kule Kasigau, kupitia mradi wa Wildlife Works REDD+, tuna njia ya kutunza misitu na kusaidia binadamu kukaa pamoja na wanyama pori. Kupitia kazi ya REDD+, tunaweza kufadhili mahitaji yetu kama vile elimu, ufikiaji wa maji safi na kliniki.  Kupitia ufadhili wa masomo, wanafunzi wameenda kusoma na sasa wanarejea kwenye jamii kama walimu, nesi, madaktari na wamiliki wa biashara.

>100k

JAMII
WASHIRIKA

200k

HEKARI
ZA MISITU ZILIZOLINDWA

11

SPISHI ZILIZO HATARINI
ZILILINDWA

1.8m

YA UCHAFUZI WA tCO2e
IMEZUIWA KUFIKIA SASA

TAZAMA

KUHUSU MRADI WA REDD+ WA KASIGAU CORRIDOR
The Kasigau Corridor REDD+ project is the world’s first and longest standing certified REDD+ (Reducing Emissions from Deforestation and Degradation) project.
MAJI NI MAISHA
At the Kasigau Corridor REDD+ project in Kenya, community members are investing carbon revenue into improving access to water for all.
PICHA YA MWANAMISITU: CONNIE
At the Kasigau Corridor REDD+ project in Kenya, Connie Mwandaa has helped pave the way for female rangers.
Filip-C-Agoo-Everland-Marketing-Kenya-1670-WEB-low-resolution.jpg

KASIGAU, KENYA

logo

THE DETAILS

START DATE: JANUARY, 2010

DURATION: 30 YEARS

PROJECT TYPE: AVOIDED DEFORESTATION REDD+

METHODOLOGY: VM0009

REGISTRY: VERRA

THIRD-PARTY VERIFIED ☑

THE DETAILS

FOR DETAILS INCLUDING THE PROJECT BASELINE AND REFERENCE AREA.

READ THE FULL PROJECT FAQ FOR DETAILS INCLUDING THE PROJECT BASELINE AND REFERENCE AREA.

decorative vector image
decorative vector image
decorative vector image
decorative vector image

MAHABARI YA KUPIMA AFYA ILIFANYIWA UKARABATI NA MIPANGO YA AFYA YA BAADA YA SHULE KUWEKWA KWA ZAIDI YA WANAFUNZI 1200

ZAIDI YA MIRADI 50 YA MAJI SAFI NA UHIFADHI WA MAJI ILIKAMILISHWA

SHULE 36 ZILIBORESHWA, SHULE 10 MPYA ZILIJENGWA, NA ZAIDI YA UFADHILI 30,000 WA MASOMO KUTOLEWA

WANAWAKE 1,700 WALISHIRIKI KWENYE SHUGHULI YA UFUMAJI ILIYOZALISHA MAPATO YA $250,000 MNAMO 2021

ZAIDI YA WATU 400 KUTOKA KWENYE JAMII WALIAJIRIWA, 1/3 WAKIWA WANAWAKE

MAANGAZIO

YA ATHARI

Eneo la mradi wa Kasigau Corridor ni nyumbani kwa zaidi ya wanachama 100,000 wa jamii za misitu ambao wamesambaa katika miji 6.

Eneo la mradi wa Kasigau REDD+ ni nyumbani kwa zaidi ya wanachama 100,000.  Sehemu kubwa la eneo hili ni nyumbani kwa watu ambao wanajitambulisha kama Wataifa. Wataifa wanagawiwa katika makundi 3 madogo: Wadawida, Wasaghalla na Wataveta, ambao wote inasemekana huwa walihamia eneo hili karibu 1000-1300 CE.

Kijadi, Wataita waliishi milimani, karibu na vyanzo vya maji.    Hali hii iliwezesha kuwepo kwa amani kati ya idadi kubwa ya wanyama pori walioishi katika maeneo ya tambarare yaliyo chini.

Shughuli za kiuchumi za jadi zilijumuisha, uwindaji, ufugaji wa mifugo na kilimo cha matumizi ya nyumbani (mazao kama vile mtama, wawele na viazi vikuu). Kadri idadi ya watu ilivyokua na ushindani wa kutafuta rasilimali kuongezeka, Wataifa wengi walihamia maeneo ya tambarare yaliyo chini na kusababisha ongezeko la mgogoro kati ya wanyama pori ambao wanatembea huru katika maeneo haya tambarare.

Mradi wa REDD+ wa Kasigau Corridor upo katikati ya njia maarufu ya reli ya Mombasa-Nairobi, ambayo inapita katikati ya mazingira ya eneo kuu la Tsavo. Kwa kuwa karibu na njia hii muhimu ya biashara, jamii zilizo katika eneo hili zimeishi nyakati za biashara ya binadamu, ukoloni wa Waingereza, vita vya pili vya Dunia na makabiliano ya Mau Mau.

MAKALA YA 01

Mwanawe Jangili, mwenye umri wa miaka 26 Atimiza Ndoto ya Kuwa Rubani wa Uhifadhi

Daniel Zima si mtu wa kawaida. Akiwa rubani wa helikopta ndogo nyepesi ya Wildlife Works, jamaa huyu mwenye umri wa miaka 26 ametimiza ndoto zake na hata zaidi ya hayo, amejitolea kuhamasisha jamii yake.

Soma zaidi

MAKALA YA 02

Masimulizi ya Ufanisi ya Ufadhili wa Masomo


“Kutoka katika hali ambapo hakukuwa na matumaini ya siku za baadaye hadi nilipo leo ni mafanikio yangu makubwa," asema Julius Mkala, aliyenufaika na mpango wa ufadhili wa masomo wa Wildlife Works.

Soma zaidi

MASIMULIZI YA JAMII

UZALISHAJI WA MAKAA YA KIMAZINGIRA

Pata maelezo zaidi

Uchomaji wa makaa unaweza kuharibu sana mazingira, kwa kuwa inahitaji tani 10 ya mbao kuzalisha tani 1 ya makaa.   Timu yetu endelevu ya kushughulikia makaa imezalisha mamia ya maelfu ya kilogramu za makaa za kimazingira bila kukata hata mti mmoja na zinatengeneza njia za mauzo ili kuongeza usambazaji wake. Wafanyakazi nane wa kudumu wanachakati matofali ya makaa 850-1,274 ya kilogramu 0.5 kila wiki.

​UTAWALA WA JAMII
Pata maelezo zaidi

Kamati za Hewakaa za Kimaeneo (LCC) ni mfumo wa utawala ambao jamii inatumia kugawa moja kwa moja mapato ya hewakaa kuelekea mipango inayoendeshwa na jamii. LCC huchaguliwa kwa njia ya kidemokrasia na huidhinisha matumizi ya bajeti kwenye miradi mbalimbali ya jamii.

USAWA KATIKA ELIMU
Pata maelezo zaidi

Kando na ufadhili wa mipango ya masomo na miundombinu ya shule, jamii zimechagua kutumia mapato ya hewakaa kufadhili mipango ya elimu ya afya ya baada ya shule. Mnamo 2021, mpango wa majaribio ulizinduliwa katika shule 10 za msingi katika eneo zima la mradi, ambao ulijumuisha spoti ya jinsia zote ya voliboli na elimu kuhusu afya ya uzazi. Mada zilizofundishwa, kwa wasichana kwa wavulana, ni pamoja na dhuluma za kijinsia, hedhi, magonjwa ya zinaa na virusi vya HIV.

AJIRA ENDELEVU
Pata maelezo zaidi

Mradi ulisaidia makundi ya wanawake wanaofuma vikapu katika eneo la mradi, pamoja na uzalishaji wa sanaa nyingine za kimazingira kama vile sabuni na mavazi, kuimarisha nafasi za kiuchumi kwa wanawake, kuwaunganisha na masoko ya nje, kukuza uwezo na kuimarisha ubora wa bidhaa za makundi ya usanifu wa ndani. 

KILIMO CHA KUHIFADHI MAZINGIRA
Pata maelezo zaidi

Vivungulio vyetu husambaza miche kwa jamii kwa ajili ya upanzi wa miti mingine kwenye misitu na bustani za jamii. Mapato ya hewakaa pia inafadhili ufikiaji wa maji na mafunzo ya kilimo endelevu.

UHIFADHI WA MAJI
Pata maelezo zaidi

Mapato ya kaboni yamefadhili kukamilishwa kwa miradi ya miundombinu ya maji (maeneo ya kuvutia mvua, mabomba, n.k) ambayo huimarisha ufikiaji wa maji safi kwa zaidi ya watu 100,000.

WASHIRIKA

WA JAMII

° Loxodonta africana

NDOVU WA SAVANA YA AFRIKA

Ndovu wa savana wa Afrika, ni wanyama wakubwa zaidi kwenye sayari yetu, pia ni baadhi ya wanyama wa kuhamasisha sana. Kumbukumbu zao za ajabu zinawaisaidia kukumbuka maeneo muhimu ya lishe wanapozuru savana. Umahiri wao kihisia na ukarimu huwafanya kuwa na makundi ya karibu kijamii nyakati za majanga. Wana maisha mazuri kijamii, yaliyojaa matukio ya furaha na vipindi vya majonzi (au "matanga ya ndovu") wanapoondokewa na wenzao kundini. Ndovu wa Afrika wanafahamika kama "wahandisi wa mazingira" kwa sababu wanaunda makazi ya kipekee kwa spishi nyingine kwa kubadilisha mazingira halisi. Kupitia miguu yao mikubwa, wanaweza kuunda vidimbwi vya maji kwa ajili ya vyura. Pia wanaweza kusaidia kurutubisha udongo na kueneza mbegu za mimea ambayo wanakula, na kuchangia kwa njia chanya maisha katika mazingira. Mgogoro kati ya binadamu na wanyama sasa ni mojawapo ya matishio kwa ndovu wa Savana kote barani Afrika, ambao idadi yao imepungua kwa angalau asilimia 60 katika kipindi cha miaka 50 iliyopita, kwa mujibu wa tathmnini za hizi punde za IUCN. Ukame unaosababishwa na mabadiliko ya tabianchi pia uneibuka kama tishio kwa ndovu Maafisa wa wanyama pori wa Kenya hivi majuzi walirioti kwamba ukame sasa unauma 20 zaidi ya ndovu kuliko ujangili, huku ndovu 179 wakikufa kutokana na kukosa maji katika nusu ya kwanza tu ya 2022. Idadi inayokadiriwa ya 11,000 hutumia mkondo huu kama njia muhimu ya kuhama, na zaidi ya ndovu 2,000 wanatumia nafasi hiyo kama makao ya kudumu.

° Giraffa tippelskirchi 

TWIGA WA MAASAI

Twiga, wanyama wakuu wanyamavu wa savana, ni nguzo katika mazingira salama kwenye mradi wetu wa Kasigau Corridor. Kwa kutumia mashingo yao marefu ya futi 6, twiga wanaweza kula na kukata majani yaliyo juu zaisi ya miti ya kipekee yenye miiba ya mgunga. Kwa njia hii, twiga hawashindani na wanyama wengine wadogo wala nyasi na majani kupata chakula, na hufungua sehemu za juu za miti ili mimea iliyo chini iweze kupata mwangaza. Katika kufanya hivyo, twiga husaidia kueneza mbegu za migunga kwenye eneo zima la savana wanapohama. Katika miaka 30 iliyopita, idadi ya twiga kote barani Afrika imepungua kwa zaidi ya 40% na sasa kuna takriban twiga 100,000 waliosalia barani Afrika. Matukio ya ukame ambayo yamesababishwa na mabadiliko ya tabianchi, kupotea na kugawanywa kwa makao, uwindaji na ujangili unaolenga ngozi na mikia ya twiga yote ni mambo yanayochangia kupungua kwao.

° Panthera leo

SIMBA

Simba ni wanyama bingwa wa kuwinda wenzao, na hufanya jukumu kubwa la kudhibiti idadi ya wanyama wala nyasi na majani. Bila simba, mazingira hayawezi kuwa na usawa, na idadi za juu kupindukia za punda milia, swara na paa bila shaka hula nyasi kupita kiasi na kusababisha uharibifu wa makao. Kwa kuwafuata na kuwauwa wanachama wadhaifu zaidi kwenye kundi (ambao mara nyingi hubeba wadudu, magonjwa au ulemavu wa kijenetiki) simba husaidia kudumisha idadi salama na stahimilivu na kuzuia kuenea kwa magonjwa. Licha ya umuhimu huu, idadi ya simba imezidi kudidimia kote duniani kutokana na ujangili na kupoteza makao kutokana na shughuli za binadamu. Kote duniani, inakadiriwa kuwa simba waliokomaa waliobaki ni kati ya 30-40,000 barani Afrika, na wameorodheshwa kama Walio hatarini kupotea kwenye IUCN. Wakati wowote ule, kuna simba 15 hadi 30 katika eneo la mradi wetu.

° Gyps africanus

TAI MWENYE MGONGO MWEUPE

Tai mwenye mgongo mweupe, ni spishi muhimu aliye hatarini katika eneo letu linalolindwa nchini Kenya, ni muhimu katika kudumisha afya ya mazingira. Huenda isiwe kazi yenye hadhi sana, lakini kama "jamaa wa taka" wa Savana, tai huondoa uchafu kwenye mazingira ambao una madhara kwa binadamu na spishi nyingine. Licha ya umuhimu huu, asilimia 70 ya spishi zote za tai wa Afrika zipo hatarini. Baadhi ya dawa za mifugo, kama vile Diclofenac, ni hatari kwa tai wanaokula mizoga yao. Wakati mwingine tai hupewa sumu kimakusudi na majangili ambao hawataki ndege hao kuonyesha mahali ambapo mnyama ameuawa kwa njia haramu. Kupotea kwa tai kunaathiri mfumo wa chakula na kuathiri vibaya spishi nyingi, ikiwa ni pamoja na binadamu. Bila tai, wanyama wengine kama vile fanya na mbwa inaweza kujaza mazingira yake, hali inayoweza kusababisha magonjwa kuenezwa kwa na katika hali fulani, kuuwa binadamu. Katika kesi ya tai, ni wazi kwamba wanyama pori hufanya kazi ili kudumisha mazingira na afya ya binadamu. Kwa ushirikiano na jamii za ndani, tumejitolea kulinda spishi zilizo hatarini za tai na maskani yao ya Kasigau Corridor.

MUHIMU
SPISHI ZA WANYAMA PORI

Eneo la mradi sasa ni nyumbani kwa wanyama pori wengi ajabu ikijumuisha zaidi ya spishi 300 za ndege, spishi 20 za popo, na zaidi ya spishi 50 za wanyama wakubwa ikiwa ni pamoja na idadi muhimu ya spishi zilizo kwenye Orodha Nyekundu ya IUCN kama vile Punda Milia wa Grevy na Mbwa wa Mwituni mwenye asili ya Afrika.

Kasigau Corridor ina zaidi ya hekari 200,000 za msitu wa Mgunga-Commiphora wa maeneo makavu

Wanajamii wengi wanategemea miti ya Migunga na Commiphora kutengeneza makaa, ambayo hutumika kupika mlo. Kiwanda chetu cha makaa ya mazingira sasa kinasaidia kutengeneza makaa kwa njia endelevu bila kukata miti, na kwa sasa kinazalisha takriban matofali ya elfu moja ya makaa ya kilogramu 0.5 kwa wiki.

Mti wa kipekee wa mbuyu (almaarufu Mti wa Maisha) unapatikana kila mahali kwenye Kasigau Corridor. Kama mti mkubwa zaidi duniani wenye maji, pia unaweza kuhifadhi zaidi ya galoni 1000 ya maji kwenye shina lake na unaweza kuishi kwa zaidi ya miaka elfu moja. Mti wa mbuyu husaidia kutoa kivuli na makao muhimu kwa wanyama pori na ni muhimu kwa desturi za kitamaduni za jamii za ndani.

​MISITU

MAI NDOMBE

 DRC

Katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), mradi wa REDD+ wa Mai Ndombe hulinda hekari 300,000 za msitu.

Pata maelezo zaidi

ENEO LA KIMAZINGIRA LA PASIFIKI KOLOMBIA

Katika Eneo la Kimazingira la Pwani ya Pasifiki ya Kolombia, tuna miradi 3 inayoendelea ya kulinda heakri 500,000 ya misitu.

Pata maelezo zaidi

GUNDUA MIRADI YETU MINGINE

ASILI

Mradi wa REDD+ wa Kasigau Corridor unatumika kama njia muhimu ya wanyama pori kati ya nusu mbili za mbuga kubwa zaidi la wanyama nchini Kenya: Tsavo Mashariki na Tsavo Maghribi.

Mwishoni mwa miaka ya 1990, msitu wa eneo kavu la Kasigau Corridor uliharibiwa kupitia mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na kutumiwa kama malisho kupita kiasi, kukata na kuondoa miti ili kuchomea makaa na wawindaji haramu kufikia ardhi hiyo. Miongo kadhaa ya matumizi mabaya na kutengwa kuliwachosha wanajamii wa maeneo haya, na ari yao ya kukidhi mahitaji yao ya kimsingi ilifanya waishi maisha isiyo ya kudumu ambayo iliharibu mazingira yale ambayo walitegemea.

MRADI

Kupitia mradi huu wa kimsingi, Wildlife Works ilivunja mipaka ya mfumo wa jadi wa uhifadhi wa mazingira, na kuwa mstari wa mbele wa kuunda njia mpya ya kuhifadhi mazingira: njia ambapo inaipa jamii nafasi ya mbele katika kufanya maamuzi.  Lengo la mradi huu ilikuwa ni kupunguza shinikizo kwenye mazingira kupitia uundaji wa nafasi za ajira.
 
Kwa kulinda misitu na kuchuma mapato kutokana na mauzo ya hewakaa, tunashirikiana na wanajamii za ndani katika eneo la Kasigau Corridor kuunda nafasi za kudumu za ajira na kuchukua nafasi ya vyanzo vya mapato visivyo endelevu kama vile ujangili, kilimo cha matumizi ya nyumbani na uvunaji wa miti kwa njia isiyo halali. Hii ni pamoja na kazi zinazolinda wanyama pori, kuunda bidhaa zinazofaa kwenye mazingira, kuwezesha elimu na kuunda kwa pamoja mbinu za kuhifadhi mazingira kupitia kilimo pamoja na wakulima.

 

Kupitia muundo wa kiuvumbuzi wa utawala wa jamii, jamii zilizo katika Kasigau ziliweka vipaumbele vyao binafsi vya kutumia mapato kutokana na hewakaa, na kusababisha uwekezaji wa kila mara katika mipango ya ufadhili wa masomo ya watoto, miundombinu shuleni, miundombinu ya maji na mipango mingine ya kuboresha uchumi, afya na ustawi wa jamii.  Learn more about    the impacts, community, wildlife, and forest of this project in the sections below.   For detailed information on the verification, third-party validation, and historic issuances of this project, see the Useful Links section,  or explore the Frequently Asked Questions section.

bottom of page