Chief Nkonsango Ndala
MWAKILISHI WA KAMATI YA HEWAKAA WA ENEO LA IBALI KATIKA MRADI WA WILDLIFE WORKS MAI NDOMBE REDD+
Hospitali na maji safi zimeboresha pakubwa afya katika kijiji chetu, na tunatazamia kujenga shule mpya hivi karibuni. Pia tunashukuru kwamba Wildlife Works imejitolea kwa muda mrefu, si kama baadhi ya wadau wengine ambao wanachangia tu bidhaa mahususi, kama vile pampu yetu ya zamani ya maji iliyoharibika, kisha wanaondoka.
TAZAMA
>50k
JAMII
WASHIRIKA
300k
HEKARI
ZA MISITU ZILIZOLINDWA
3
SPISHI ZILIZO HATARINI
ZILILINDWA
2.8m
YA UCHAFUZI WA tCO2e
IMEZUIWA KUFIKIA SASA
POACHER TO PROTECTOR
The Mai Ndombe REDD+ Project in the DRC employs over 20 eco-guardians, many of whom are former poachers.
KUHUSU MRADI WA REDD+ WA MAI NDOMBE
The Mai Ndombe REDD+ Project protects 300,000 hectares of critical bonobo and forest elephant habitat within the world’s second-largest intact rainforest and some of the most important wetlands on the planet, the Congo Basin.
MAI NDOMBE
JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO
REDD+ PROJECT SPECIFICS
START DATE: MARCH, 2011
DURATION: 30 YEARS
PROJECT TYPE: AVOIDED DEFORESTATION REDD+
METHODOLOGY: VM0009
REGISTRY: VERRA
THIRD-PARTY VERIFIED ☑
THE DETAILS
FOR DETAILS INCLUDING THE PROJECT BASELINE AND REFERENCE AREA.
READ THE FULL PROJECT FAQ FOR DETAILS INCLUDING THE PROJECT BASELINE AND REFERENCE AREA.
KLINIKI 18 ZA KUHAMISHA NA HOSPITALI MOJA KUU ILIJENGWA
SHULE 12 ZILIJENGWA AU KUFANYIWA UKARABATI
VIDIMBWI 10 VYA KUFUGIA SAMAKI VILIUNDWA NA AINA MPYA ZA MIHOGO KUANZA KUKUZWA ILI KUIMARISHA UTOSHELEVU WA CHAKULA
MAENEO 11 YENYE MAJI SAFI NA ENDELEVU YANAYOTUMIA SOLA
ZAIDI YA NAFASI 300 ZA AJIRA ZILIUNDWA
MAANGAZIO YA ATHARI
Eneo la mradi wa Mai Ndombe ni nyumbani wa wanajamii 50,000 wa misitu ambao wamesambaa kwenye zaidi ya vijiji 28.
Vijiji vingi ni nyumbani kwa watu wanaojitambulisha kuwa Wabantu. Wabantu ni wahamiaji ambao ni wafugaji mifugo, walioishi karibu na Ziwa Mai Ndombe vizazi vingi vilivyopita. Kuna kijiji kimoja nje ya eneo la mradi lakini ndani ya ukanda wa mradi ambacho ni nyumbani kwa Batwa, ambao wanafahamika zaidi kwa jina la kibaguzi la "mbilikimo." Batwa ndio walinzi asili na Wenyeji wa misitu huo.
Kutokana na miongo mingi ya ukoloni na dhuluma, wanajamii zote ndani ya eneo la mradi na ukanda wa mradi wametengwa na uwezeshaji wa kiuchumi na kisiasa na ni mojawapo ya jamii zilizotengwa zaidi ulimwenguni. Wanatafuta mikakati mipya ya kukidhi mahitaji yao ya kimsingi huku bado wakiishi kwa amani na msitu ambao wana uhusiano thabiti wa kitamaduni na kiroho nao.
MAKALA YA 01
KUREJEA KWA
NDOVU WA MISITU
Kwa miaka, mandhari ya eneo la mradi hayakuwa na wanyama pori wengi. Lakini sasa, msitu na wanyama pori wanarejea tena kutokana na mradi wa REDD+.
MAKALA YA 0202
MAHOJIANO NA
MATTHIEU BOLAA
Mathieu “De la Forêt” Bolaa Ni Mkuu wa Viumbe Anuwai katika Wildlife Works nchini DRC, na mwenyewe ameshuhudia kurejea kwa ndovu katika eneo hilo.
MASIMULIZI YA
JAMII
ELIMU
Pata maelezo zaidi
Wakiwa na mapato kutokana na hewakaa, jamii zinawekeza katika kujenga vituo vya elimu, ambavyoawali havikuwepo au havikuwa vya kutosha katika vijiji vingi kwenye ukanda wa mradi. Ukosefu wa elimu katika eneo hilo umehusiana moja kwa moja na shughuli za ukataji wa miti na matokeo mabaya ya afya. Kwa jumla, shule 32 zinapangiwa kujengwa katika kipindi kizima cha mradi. Mapato kutokana na hewakaa pia yanagharamia sare, karo za shule, mishahara ya walimu na ada za mtihani wa kitaifa.
KUONGEZA UTOSHELEVU WA CHAKULA
Pata maelezo zaidi
Ziwa Mai Ndombe ni mojawapo ya maziwa ya kipekee zaidi kibayolojia duniani. Tofauti na maziwa mengi makubwa ya Afrika, spishi nyingi za samaki hazijawai kuwekwa hapa, hali iliyosababisha makazi yenye ukwasi wa spishi za kimaeneo. Laini katika miongo kadhaa iliyopita, idadi ya samaki imepungua sana kutokana na shughuli zisizoendelevu za uvuvi. Wanajamii wamewekeza mapato yanayotokana na hewakaa kwenye vidimbwi endelevu vya samaki ili kuimarisha utoshelevu wa chakula na hatimaye kuongeza idadi ya samaki kwenye ziwa.
TIBA BORA
Pata maelezo zaidi
Matibabu yaliyoboresha ni mojawapo ya shughuli muhimu za mradi huu ambazo jamii katika Mai Ndombe REDD+ huwekeza mapato yao ya hewakaa. Viwango vya vifo vya kina mama wajawazito ni mojawapo ya vya juu zaidi duniani na ⅓ ya watoto wenye umri wa chini ya miaka 5 hawana chakula cha kutosha na wengi wapo katika hatari ya kuambukizwa maleria na ukambi. Hospitali mpya na kliniki tamba za kujibu haraka zinabadilisha ufikiaji wa tiba bora ya afya.
UTAWALA WA JAMII
Kamati za Maendeleo za Eneo zimewekwa kama mfumo muhimu wa utawala wa ndani ya eneo la mradi. Shughuli za mradi huchaguliwa kwa ushauriano na kamati za ndani pamoja na washikadau wengine muhimu na maafisa kutoka viwango tofauti vya serikali.
MAJI SAFI
Pata maelezo zaidi
Tulichuma mapato kutokana na hewakaa kutoka ulinzi wa misitu, jamii zimewekeza kwenye mashine zinazobebeka za kuchimba ili kutafuta maji safi.
KILIMO CHA KUHIFADHI MAZINGIRA
Pata maelezo zaidi
Mihogo ni chakula muhimu kwa mamilioni ya watu kote nchini DRC, lakini uzalishaji wake unatishiwa na wadudu na magonjwa mengi.
Wafanyakazi walioajiriwa kutoka katika eneo hilo hutunza bustani, hufanya kilimo cha msituni na kutoa mafunzo ya ukulima wa kuhifadhi mazingira ili kuongeza ufikiaji wa taarifa kwa wanajamii ili waweze kuboresha mazao yao kwa njia endelevu.
WASHIRIKA
WA JAMII
° Pan paniscus
BONOBO
Bonobo wanahusiana na binadamu kwa takriban asilimia 98.7, na kuwafanya kuwa jamaa zetu wa karibu zaidi. Wanapatikana tu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na eneo la mradi wetu kule Mai Ndombe ni mahali muhimu kwa spishi hizi zilizo hatarini kukimbilia usalama wao. Matishio makubwa kwa bonobo ni kupoteza makazi na masoko haramu ya biashara ya wanyama pori. Bonobo huwindwa kwa ajili ya nyama yao au kuuzwa kama wanyama vipendwa. Kutokana na usumbufu kutoka kwa kampuni ya awali ya kutengeneza mbao, kulikuwa na bonobo 20 hadi 30 wakati tulianza mradi wetu. Leo, kuna bonobo 15-20,000 katika eneo la mradi wetu wakati wowote ule. Hii ni muhimu kwa ukuaji wa spishi hii kwa ujumla, kwa kuwa kuna tu idadi inayokadiriwa ya bonobo 30-50,000 msituni.
° Loxodonta cyclotis
NDOVU WA MISITU
Ndovu wa misituni ni wadogo na wapweke zaidi ikilinganishwa na binamu zao wakubwa wa Savana. Ilikuwa ni mwaka 2021 ambapo ndovu wa msituni walitangazwa kuwa spishi tofauti. Kama watunza bustani wakuu wa mwituni, Ndovu wa misituni ni mojawapo wa wapiganaji bora zaidi dhidi ya mabadiliko ya tabianchi. Kwa kula mimea midogo, ndovu hupunguza ushandani wa lishe ya udongoni na mwangaza, hali inayowezesha miti mikubwa kunawiri na kunasa kiasi kikubwa cha Hewakaa ya CO2 hewani. Wanasayansi wanasema kwamba kuwepo kwa mnyama mkubwa mla nyasi ndio sababu ya Ukanda wa Kongo inachukua maradufu ya kiasi cha hewakaa kuliko msitu wa Amazon licha ya kwamba ni nusu yake tu kwa ukubwa. Matishio makubwa kwa ndovu wa msituni ni mabadiliko ya tabianchi, kupoteza makao, ujangili wa kutafuta pembe, na mauaji ya kulipiza kisasi kutokana na mgogoro kati ya binadamu na ndovu. Kabla ya mradi wa uhifadhi wa Wildlife Works, ndovu wa misitu hakuwa wameonekana katika eneo hilo kwa miaka mingi. Leo, idadi ya ndovu wanaopatikana huko imeongezeka na eneo la mradi sasa lina takriban ndovu 100 wa misitu.
° Smutsia gigantea
KAKAKUONA MKUBWA
Kakakuona, wenye magamba na pua refu, wanaokula sisimizi, ni mojawapo ya wanyama wa kipekee duniani. Kwa kula mchwa, wanasaidia kulinda miti na kudumisha usawa wa kiekolojia. Inasikitisha kwamba, pia ndiye mnyama ambaye walanguzi wanamuuza sana duniani, kwa sababu magamba yake yanatumika kama dawa za kienyeji katika eneo la Asia Mashariki.
° Hippopotamus amphibius
VIBOKO
Baada ya ndovu na vifaru, viboko ndio wanyama wa tatu kwa ukubwa duniani, kiboko wa kiume anaweza kuwa na uzani sama na wa magari matatu mazito. Viboko wanaweza kuwa wakali na walinzi wa himaya zao, na kwa wastani, huuwa watu 500 kwa mwaka barani Afrika (karibu mara mbili ya idadi ya watu wanaouawa na simba). Licha ya hadhi yao ya kuvutia na ukali wao, idadi yao inapungua Kusini mwa Jangwa la Sahara, zaidi kwa kasi katika nchi ya DRC. Matishio makubwa kwa viboko ni kupoteza makazi na uwindaji kwa ajili ya nyama na meno yao. Wildlife Works, kwa ushirikiano na jamii za ndani, inaweka mikakati ya wanyama hawa kuishi kwa pamoja na binadamu.
MUHIMU
SPISHI ZA WANYAMA PORI
Picha ya kamera ya tumbili aina ya bonobo (pan paniscus) katika shimo la maji kwenye eneo la mradi la Mai Ndombe REDD+
Picha ya kamera ya ndovu wa msituni (Loxodonta cyclotis) katika mradi wa Mradi wa REDD+ wa Mai Ndombe nchini DRC
Msitu huu wenye ukubwa wa ekari 740,000 kimsingi una miti inayodondosha majani katika vipindi fulani (46%) na (42%) misitu ya kinamasi.
Msitu huu ni nyumbani kwa mti mgumu wa Mwenge (Millettia laurentii), ambao kihistoria ulivutia kampuni kadhaa za viwanda vya kutengeneza mbao. Msitu huu una ukwasi wa viumbe anuwai, huku spishi nyingi za mimea ikiwa bado hazina ufafanuzi wa kisayansi. Timu yetu ya viumbe anuwai bado inaendelea kugundua spishi mpya za mimea na fungi. Ingawa ukanda wa Kongo ni nusu ya msitu wa Amazon, inatumia kiasi maradufu cha hewakaa. Hii inadhaniwa ni kwa sababu ya kuwepo kwa wanyama wakubwa wala nyasi, kama vile ndovu wakubwa, wanaopunguza ushindani wa miti mikubwa inayovuta hewakaa hiyo.
MISITU
KASIGAU CORRIDOR
KENYA
Nchini Kenya, mradi wa REDD+ wa Kasigau Corridor hulinda hekari 500,000 za msitu.
ENEO LA KIMAZINGIRA LA AMAZON KOLOMBIA
Katika Eneo la Kimazingira la Kolombia, tuna miradi 3 tunayounda ya kulinda hekari 750,000 ya misitu.
GUNDUA MIRADI YETU MINGINE
ORIGINS
Nearly 300,000 hectares of rainforest along the west side of Lake Mai Ndombe in western DRC was zoned for commercial timber extraction that is highly valued by logging companies. The forest is home to incredible biodiversity and includes some of the most important carbon-rich wetlands in the world. The logging companies largely ignored the rights and health of the 50,000 community members. It brought little or no economic benefit to the local people and drove already threatened wildlife populations down.
In 2008, following a governmental revision of the DRC National Forest Code, 91 of 156 logging contracts were suspended in an effort to address corruption in the sector.
THE PROJECT
Two of these temporarily suspended timber concessions encompassed the rainforest along the western shore of Lake Mai Ndombe. In February 2010, a formal request was made to the DRC government to cease the destructive logging practices and instead use carbon revenues to promote environmental conservation and sustainable development. In 2011, the two concession contracts were successfully reassigned to ERA Congo (the founding project developer) via a Forest Conservation Contract. Today, ERA Congo is a fully owned and operated subsidiary of Wildlife Works managing the Mai Ndombe project under the same agreements with the DRC government.
The communities agreed to partner with Wildlife Works to co-create strategies for improved food security, access to healthcare and education, while maintaining their centuries-long tradition of living in harmony with the forest. Learn more about the impacts, community, wildlife, and forest of this project in the sections below. For detailed information on the verification, third-party validation, and historic issuances of this project, see the useful links section, or explore the Frequently Asked Questions section.