ANZISHA MRADI
Mfumo Wetu: Ufadhili wa Hewakaa Unaolenga Jamii
Ungependa kuanzisha mradi wa REDD+? Wildlife Works inapata ufadhili kamili ili kuanzisha miradi mipya ya misitu ambayo inatoa ufadhili wa shughuli za uhifadhi kwa jamii za msitu ili kulinda misitu yao na rasilimali za hewakaa. Ikiwa una mradi wa msitu ambayo ungependa kuzingatia, tunatafuta miradi mipya ya misitu ambayo itakidhi vigezo vifuatavyo:
-
Eneo pana la msitu lenye hifadhi nzuri ya hewakaa, na uwezekano wa kulipanua kadri muda unavyosonga.
-
Jamii ambayo itanufaika kutokana na mradi wa REDD+, (tunaamini kuwa jamii za misitu ni muhimu katika kukomesha ukataji wa miti). Pia tunafikiri kuwa jamii zinapaswa kumiliki hifadhi zao za hewakaa. Mapato yanayotokana na hewkaa yanapaswa kurudi kwenye jamii ili kulinda misitu, kulinda afya ya jamii, elimu, kuwezesha kina mama na mahitaji mengine yatakayobainisha katika mchakato wa washikadau wa jamii).
Kando na hayo tunatafuta:
-
Washirika wa NGO ambao wanafahamu eneo husika na wamefanya kazi na jamii za hapo.
-
Serikali zilizo tayari kugundua REDD+ kama sehemu ya juhudi zao za kukomesha mabadiliko ya tabianchi na kusaidia katika kuunda nafasi za ajira kwa jamii za eneo husika wanaosaidia katika uhifadhi wa mifumo ya mazingira ya vizazi hadi vizazi.
-
Maeneo ya misitu yenye thamani ya juu ya uhifadhi au thamani ya viumbe anuwai.
-
Maeneo ya misitu yanayoweza kutumiwa kama njia au maeneo salama ya urejeshaji wa wanyama pori.
-
Maeneo ya misitu yanayoelekea kukatwa, ambayo yanaweza kulindwa kupitia REDD+.
Ikiwa nyinyi ni jamii, serikali au NGO na mna eneo mahususi la misitu panapofaa mradi wa REDD+, tafadhali wasiliana nasi kupitia mada ya "mradi mpya". Tutakujibu ndani ya saa 48. Tafadhali jumuisha Mradi Mpya kwenye mada ya baruapepe yako.